Burudani

Wakazi: Muziki haufunikwi na siasa

Watu wengi kwa sasa hapa nchini wanaamini muziki wa Bongo Fleva unafichwa kutokana na habari za siasa kutawala sana kwenye vyombo vya habari kuliko muziki.

Hali hii inawapa hofu pia wasanii wengi kutoa nyimbo zao wakiamini hazitapewa nafasi ya kusikilizwa na hata siku za hivi karibuni mazungumzo ya mtandaoni kati ya Diamond Platnumz na Shetta yalionyesha hilo pia(japo huenda walikuwa wakitaniana).

Kwenye Interview na Prince Ramalove kupitia Kings Fm, rapper Wakazi ametofautiana na wengi kwa kudai kuwa sio kweli kwamba muziki unafunikwa na siasa.

“Siasa ipo kila siku hata kama kuna muziki au hamna muziki,sema aina ya muziki fulani inakua inafanya vizuri zaidi na ina relate na watu kutokana na kinachoendelea katika jamii kwa muda huo,na hiyo ndio siasa yenyewe,” amesema Wakazi.

Pia rapper huyo amedai kuwa kama msanii una muziki mzuri, utaendelea kufanya vizuri siku zote.

By Prince Ramalove
Kings Fm(Njombe)

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents