Tupo Nawe

Wakenya hawakamatiki kwenye riadha, Mwingine aweka rekodi mpya duniani (+video)

Mwanariadha kutoka nchini Kenya, Geoffrey Kamworor (26) amevunja rekodi ya dunia katika mbio ndefu za Copenhagen Half Marathon, zilizofanyika leo Jumapili Septemba 15, 2019 nchini Denmark.

Geoffrey Kamworor

Kwenye mbio hizo za kilometa 21, Kamworor alitumia muda wa dakika 57:01. Na kuweka rekodi mpya ya kutumia muda mfupi zaidi wa Half Marathon duniani.Image

Kamworor ambaye ni bingwa mara tatu wa mbio hizo, Amevunja rekodi ya Mkenya mwenzie, Abraham Kiptum ya kukimbia umbali huo kwa dakika 58.01, Ambayo aliiweka katika mbio za Valencia Half Marathon mwezi Oktoba mwaka jana.

Tayari shirikisho la riadha ulimwenguni (IAAF). Limeiweka rekodi hiyo mpya ambayo ilikuwa inashikiliwa na Abraham Kiptum kwa muda wa dakika 58:18.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW