Afya

Wakenya waanza kutekeleza amri ya kutotoka nje usiku kisa virusi vya Corona, Polisi watumia nguvu kuwazuia – Video

Wakenya waanza kutekeleza amri ya kutotoka nje usiku kisa virusi vya Corona, Polisi watumia nguvu kuwazuia - Video

Amri ya kutotoka nje cnini kenya kuanzia 7 moja usiku hadi saa kumi na moja alfajiri imeanza kutekelezwa mwendo wa saa moja huku huku wafanyakazi wa huduma muhimu pekee wakiruhusiwa kuwa nje usiku.

Hatua hiyo inalenga kuwazuia Wakenya kutangamana katika makundi ya watu nyakati za usiku ili kuzuia kuenea kwa virusi vya ugonjwa wa corona ambavyo tayari vimewaathiri watu 31 huku mtu mmoja akidaiwa kufariki siku ya Alhamisi.

Mwendo wa saa kumi na mbili jioni, Wakenya wengi mjini Nairobi walionekana wakiharakisha kuelekea nyumbani hatua iliosababisha msongamano katika barabara kadhaa huku wale waliokuwa wakitumia magari ya umma wakionekana kusubiri katika vituo vya magari hayo licha ya muda kuyoyoma.

Matatu chache zilizokuwepo zilitumia fursa hiyo kujitengezea fedha baada ya kuongeza nauli huku baadhi yazo zikikiuka agizo jipya la kupunguza idadi ya abiria ndani ya magari hayo ili kuwaepusha dhidi ya maambukizi ya virusi vya corona.

Hatahivyo wengine wao walikata kauli na kuanza kutembea kwa miguu wakihofia kukamatwa na maafisa wa polisi.

Inspekta jenerali wa polisi siku ya Ijumaa alionya kwamba wale watakaopatikana nje ya nyumba zao baada ya saa moja usiku watakabiliwa iwezekanavyo.

Mjini Mombasa na Eldoret hatahivyo mpango huo uilianza kwa mkosi baada ya maafisa wa polisi kukabiliana na wakaazi saa mbili kabla ya amri hiyo kuanza kutekelezwa.

Barabara nyingi za mji wa Nairobi zilisalia kuwa mahame mda mfupi kabla ya amri ya kutotoka nje kuanza kutekelezwa
Image captionBarabara nyingi za mji wa Nairobi zilisalia kuwa mahame dakika 30 kabla ya amri ya kutotoka nje kuanza kutekelezwa
Barabara nyingi za mji wa Nairobi zilisalia kuwa mahame dakika 30 kabla ya amri ya kutotoka nje kuanza kutekelezwa
Image captionBarabara nyingi za mji wa Nairobi zilisalia kuwa mahame dakika 30 kabla ya amri ya kutotoka nje kuanza kutekelezwa
Msongamano wa magari huku Wakenya wakiwania kwenda majumbano mwao muda mchache kabla ya amri ya kutotoka nje kutekelezwa
Image captionMsongamano wa magari huku Wakenya wakiwania kwenda majumbano mwao muda mchache kabla ya amri ya kutotoka nje kutekelezwa

Hekaheka kivukoni likoni

Katika mtafaruku huo Maafisa wa polisi waliwachapa mamia ya watumiaji wa kivuko cha likoni ambao walikuwa wamepanga foleni ili kuingia katika kivuko hicho.

Maafoisa hao waliokuwa wamejihami na marungu waliwapiga abiria hao walipojaribu kutumia nguvu kuingia katika kivuko hicho.

Baadhi ya abiria hao walikuwa wakidai kwamba waikuwa wanachalewa kwenda nyumbani mapema ili kuitikia wito wa serikali wa kutumiza amri ya kutotoka nje baada ya saa moja usiku.

https://twitter.com/alhayyal12/status/1243552540815491083

https://twitter.com/alhayyal12/status/1243810562087227392

Chanzo BBC

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents