Habari

Wakenya wamkaba koo Rais Kenyatta, waanzisha kampeni ya #MrPresidentTumechoka kwenye mitandaoni ya kijamii

Kwa mujibu wa tafiti za Taasisi ya Transparency International inayoshulikia masuala ya rushwa duniani, Kenya inatajwa kuwa kila mwaka vitendo vya rushwa vinaongezeka, jambo ambalo linafanya wananchi waanze kuchukia viongozi wao kwa kutowajibika.

Rais Kenyatta kushoto kwenye picha.

Hivi karibuni, duru la habari nchini Kenya ziliripoti kwamba mabilioni ya fedha yaliyotengwa kujenga mradi wa bwawa la maji katika eneo la Bonde la ufa magharibi mwa nchi hiyo zimepotea kusikojulikana jambo ambalo limezua taharuki kwa wananchi.

Kashfa hiyo ni miongoni mwa kashfa lukuki za ufisadi nchini humo, ambapo wananchi wamekuwa wakihoji kwanini viongozi hawachukui hatua ya kuwakamata mafisadi.

Kuanzia jana nchini Kenya, Wananchi kwenye mitandao ya kijamii wamejitosa kuelezea hisia zao na kuchoshwa, kwa kile wanachotaja kuwa ni vitisho vya bure kwa viongozi dhidi ya rushwa kwani, Serikali imekuwa ikishindwa kuwachukulia hatua.

Wakenya wengi wameeleza kwamba, wanahisi Rais Kenyatta hajachukua hatua stahiki katika kupambana na rushwa, na ndio maana imezidi kukithiri.

Tayari kampeni ya #MrPresidentTumechoka imeanza ku-trend kwenye mitandao ya kijamii nchini Kenya, ikimshinikiza Rais Kenyatta aongeze juhudi katika kupambana na rushwa.

Mpaka sasa hivi, kuna kashfa kubwa nne za rushwa ambazo zinalikumba taifa hilo lenye nguvu ya kiuchumi Afrika Mashariki.

ufisdai Kenya

Kwa upande wake Rais Kenyatta, kupitia ukurasa wake wa Twitter amewataka Wakenya waungane kwa pamoja katika vita hiyo dhidi ya rushwa kwani sio vita ya mtu mmoja.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents