Soka saa 24!

Wakenya wamshambulia Rais Kenyatta mitandaoni, wadai ame-copy & paste muonekano wa sare za jeshi la polisi la China

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta amejikuta katika wakati mgumu nchini humo baada ya raia wa Taifa hilo kumuandama mitandaoni wakidai kuwa sare mpya za jeshi la polisi alizozitangaza mapema leo, ni mbaya na zinafanana na za jeshi la polisi la China.

Rais Kenyatta akisalimiana na wakuu wa vituo vya jeshi la polisi

Baadhi ya maoni ya wadau hao, wameeleza kuwa  sare hizo ni kama za China na huenda kuna hela imepigwa kwenye mradi wa ushonaji wa sare hizo.

Leo Septemba 13, 2018,  Rais Kenyatta ametangaza mabadiliko ya nafasi mbali mbali za Jeshi la Polisi nchini humo, ikiwemo na mabadiliko ya sare za Jeshi.

Pitia baadhi ya mijadala na maoni yaliyotolewa na baadhi ya Wakenya kwenye mitandao ya kijamii nchini humo.

Tayari Hashtag ya #PoliceReforms imeendelea kupata Tweets za kutosha wengi wakubeza hatua ya mabadiliko ya sare wakitaka mabadi;liko yafanyike kwenye utendaji kazi wa jeshi hilo.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW