Burudani

Wakenya washinda dola za Kimarekani 50, 000 kwenye kipindi cha Ellen Degeneres cha ‘The Ellen Show’

Familia ya Kenya imeshinda dola za Kimarekani 50,000 ambazo ni sawa na fedha za nchi hiyo ya Afrika Mashariki (Ksh.5,000,000) katika kipindi cha luninga cha mchekeshaji wa Kimarekani Ellen Degeneres’ kinachoitwa cha ‘The Ellen Show.’

Image result for Ellen Degeneres Kenya family

Zawadi hiyo ilitolewa baada ya muongozaji wa kipindi cha luninga cha Marekani Ellen Degeneres kumkutanisha Achieng’ mwanamke raia wa Kenya anayeishi Marekani na familia yake baada ya kutengana kwa miaka miwili.

Kwa mujibu wa shirika la habari la BBC, Mchekeshaji huyo alimuita studio Achieng Agutu aliyeondoka kwenda Marekani kupata elimu ya juu na baadae alimshitukiza kwa kumuunganisha na familia yake kwa njia ya simu ya video.

Achieng aliishi na familia ya muongozaji wa kipindi, inayohfahamika kama the Graces lakini anafanya kazi ya kudumu huku akiwa anaweza kuhudhuria masomo shuleni.

“Nilihamia hapa (Marekani ) karibu miaka mitano iliyopita kwa kupata elimu ya juu na mambo yamekuwa mazuri, lakini bado imekuwa ni vigumu sana kwa familia yangu nyumbani Kenya kwasababu kusema ukweli wamefanya kila wawezalo kuanzia kuuza ardhi, kuchukua mikopo ili waweza kulipa karo yangu ya shule na kuhakikisha ninaishi vizuri ,” alielezea Achieng.

Aliongeza kusema kuwa wazazi na ndugu zake wamekuwa wakisaidia zaidi ya watoto 10 wanaotoka katika familia zisizojiweza nchini Kenya kwasababu wanahisi wamebarikiwa.

Achieng’ ambaye alijawa na furaha alielezea kuwa pia anafanya kazi ya udereva katika kampuni ya Uber , kuwalea watoto, mwalimu wa kiingereza na wakati mwingine husafisha nyumba za watu na kuosha magari ili kupata pesa za ziada.

Aidha alielezea jinsi kutazama kipindi cha Ellen ilivyomsaidia kuifahamu vizuri lugha ya kiingereza.

Alisema: ”Nilijifunza lugha ya kiingereza kwa kusikiliza wasanii wa muziki kwenye kipindi cha Ellen Show, na kuandika maneno na baadae kutafuta maana ya maneno hayo, na hivyo kuzungumza vizuri maneno ya kiingereza”

Kaka yake mkubwa pia Churchill yuko nchini Afrika Kusini kutafuta maisha bora.

Baada ya hapo Ellen alijifanya anaenda kutengeneza mtambo wa mawasiliano ya video yaliyokuwa yamekatika nyuma ya jukwaa, lakini alipokaribia lango, Achieng aliiona familia yake ana kwa ana na familia kwa njia ya video. Haya yalikuwa yakiendelea huku familia ya Achieng’ ikiwa nyuma ya jukwaa.

Achieng’ alishituka sana kuona familia yake ikija jukwaani alipokuwa.

Baba yake alielezea kuwa kukutana tena kama familia ni jambo kubwa sana.

Baadae walicheza mchezo wa bahati nasibu ulioandaliwa na kampuni ya Walmart na kuchagua namba 2 ambayo huja na zawadi ya juu zaidi ya dola $50,000.

Baadhi ya Wakenya wamemkosoa Achieng

Licha ya kushinda kiwango kikubwa cha pesa, baadhi ya Wakenya kwenye mitandao ya kijamii wamemkosoa Bi Achieng’ Agutu ambaye ni mzaliwa wa kisumu nchini Kenya kwa kudai kuwa alijifunza kiingereza kupitia kipindi cha ‘The Ellen Show.’ huku wakidai hakuwa mkweli kwa hili na baadhi walidai alisema hivyo ili kujipatia pesa. Baadhi wametuma picha za kukejeli madai ya Achieng’ :

https://twitter.com/pauliddiali/status/1124193751025496065

Baadhi pia walidai familia yake inajiweza kinyume na yeye alivyojaribu kuueleza umma kupitia kipindi cha ‘The Ellen Show.’

Unaweza pia kutazama:

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents