Habari

Wakili aeleza tofauti ya kuhukumiwa kunyongwa na kunyongwa hadi kufa

Wakili wa kujitegemea, Gabriel Kambona, ametoa ufafanuzi kuhusu nini tofauti ya kuhukumiwa kunyongwa na kuhukumiwa kunyongwa mpaka kufa.

kitanzi

Ametoa ufafanuzi huo katika televisheni ya Azam TV, katika uchambuzi wa hukumu za kifo.

“Kwa mtu wa kawaida kuelewa hii adhabu hii imekuwepo toka kipindi cha ukoloni na tumeirithi kutoka Ujerumani ambao walikuwa wakiitekeleza adhabu hii ya kunyongwa mpaka kufa, wakimaanisha kwamba mtu anayethibitika kuwa ameua kwa kukusudia basi adhabu yake ni hiyo na mahakama haina uamuzi mbadala kwasababu ni sheria iliyowekwa kwa mujibu wa kifungu cha 195 cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai na sheria ya kamosa ya jinai ya Tanzania”, alisema Kambona.

Akijibu tofauti ya kuhukumiwa kunyongwa na kuhukumiwa kunyongwa mpaka kufa,” alisema:

Maana yake ni kwamba hakuna mtu anayehukumiwa kunyongwa mpaka kufa, unaweza ukanyongwa labda kamba ikakatika, itabidi wakurudishe tena,lakini kuhakikisha mpaka huyu mtu anakufa na adhabu inakuwa imefikia hapo,lakini sasa mimi naangalia katika mlengo wa katiba yetu, mlengo wa sheria zetu, mlengo wa adhabu yenyewe jinsi ilivyo,mimi sihusiki sana na adhabu ya kunyonga mpaka kufa sana”,alieleza.

“Adhabu ya kunyonga mi nadhani kifungo cha maisha kinatosha sana,naamini katiba yetu ya Tanzania ibara ya 13 ibara ndogo ya 6 kifungu d na e kinaeleza kuwa mtu kuheshimu utu wake lakini pia kutoteswa. Tunaamini pia katika utekelezaji wa hii adhabu mtu kabla hajafa anateseka kwanza kwa mujibu wa adhabu hii, lakini pia tunaamini kwamba katika kutoa maisha ni Mungu pekee ndiye anayetoa ni Mungu wakuchukua mamlaka ya hayo maisha na hii adhabu ya kunyonga mpaka kufa ikitekelezeka haiwezi kurudishwa tena,” alifafanua.

Aliongeza kuwa hukumu ya kunyongwa mpaka kufa inaanzia mahakama kuu, tofauti na adhabu nyingine ambazo mtu anaweza akawa na fursa mbalimbali lakini hii inakuwa na ngazi chache tu.

BY: EMMY MWAIPOPO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents