Habari

Wakili Dk. Ringo na aliyekuwa bosi wa TIB, Peter Noni kizimbani kwa makosa 6

Wakili wa kujitegemea, Dkt. Ringo Tenga na Wakurugenzi wa kampuni ya Six Telecom, Peter Noni na Ofisa Mkuu wa Fedha Noel Odeny Chacha na Mhandisi wa Kampuni hiyo Rashid Shamte wamefikishwa mahakamani kwa kosa kuhujumu uchumi kwa kukwepa kulipa gharama za mawasiliano.

Washtakiwa walisomewa makosa yao na Wakili wa Serikali, Jehovaness Zacharia mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Victoria Nongwa.

Wamesomewa mashtaka sita ikiwemo la utakatishaji wa fedha na kusababisha hasara ya dola milioni tatu na laki saba ni sawa Bilioni 8 na kuisababishia hasara Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA).

Baada ya washtakiwa hao kusomewa mashtaka hayo hawakuruhusiwa kuongea chochote kwa sababu Mahakama hiyo haina Mamlaka hadi Mahakama Kuu.

Hakimu Nongwa amehairisha kesi hiyo hadi Novemba 24 mwaka huu kwaajili ya kutoa uamuzi kuhusu hoja za Dk Lamwai

Kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, asema haya baada ya kuulizwa kuhusu kukamatwa kwa Wakili Ringo Tenga, Mkurugenzi Mtendaji wa zamani wa Benki ya TIB Peter Noni amesema kuwa yeye ni Kamanda wa polisi wa Kanda Maalum na si Msemaji wa Makao Makuu ya Jeshi na taarifa kuwa watu hao wanashikiliwa kwa kosa la utakatishaji wa fedha suala hilo liko kwa Wizara ya Mambo ya Ndani.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents