Habari

Wakili wa matapeli wa mtandaoni kutoka Nigeria adai Hushpuppi alitekwa na FBI

Mwanaume mmoja Mnaigeria anayeshutumiwa kwa wizi wa mamilioni ya dola na usafirishaji haramu wa pesa na nchini Marekani alitekwa nyara na FBI, wakili wake amesema.

Ramon Olorunwa Abbas – anayefahamika na wafuasi wake milioni 2.5 kwenye mtandao wake wa kijamii wa Instagram kama Ray Hushpuppi – na mshukiwa mwingine wa wizi wa kimtandao Olalekan Jacob Ponle (aka Mr Woodberry) walikamatwa mjini Dubai, ambako wanaishi mwezi Juni.

Baadae walifikishwa katika mahakama ya Chicago tarehe 3 Julai.

Muungano wa miliki za kiarabu (United Aran Emirates) hauna mkataba wa kuwasafirisha wahalifu kwenda Marekani lakini polisi ya Dubai walisema wamekwishwa wasafirisha hadi Marekani.

Msemaji wa Wizara ya sheria nchini Marekani ameiambia BBC kuwa Hushpuppi alifukuzwa kutoka Dubai na hakuletwa Marekani.

Hakujibu ni vipi alifika nchini Marekani.

Wakili wa Hushpuppi alisema nini?

Wakili wa Abbas, Gal Pissetzky ameiambia BBC kwamba mteja wake , ambaye picha zake kwenye mtandao wa Instagram zilionyesha maisha ya kifahari , hakua mhalifu na alipata pesa kwa njia halali.

“Ana ushawishi katika mitandao ya kijamii akiwa na mamilioni ya wafuasi, akiwa na mamilioni ya watu wanaompenda na kumheshimu, na anawapenda, na hicho ndicho alichokifanya.

Katika jamii ya sasa, hiyo ni biashara,” alisema.

Bwana Pissetzky anakiri kwamba hafahamu “kwa 100% ” masuala ya mitandao ya kijamii na watoto wake walimwambia kuwa ni mtu mzima sana lakini ana fahamu “hivyo ndivyo watu wanavyotengeneza pesa siku hizi.

Transparent line

Hoja ya wakili wa mshitakiwa wa Chcago ilikuwa kwamba Hushpuppi alilipwa na nembo za mitindo ya mavazi katika kesi hiyo inayotarajiwa kuchukua muda mrefu katika mahakama ya Marekani.

Shirika la upelelezi la Marekani (FBI) linamshutumu Bwana Abbas, mwenye umri wa miaka 37, kwa kuhusika katika wizi wa pesa wa mamilioni ya dola kwa njia ya barua pepe na mifumo mingine ya wizi.

Je Marekani ilitimiza sheria ?

Ni kesi kubwa zaidi ya wizi inayomuhusisha raia wa Nigeria nchini Marekani lakini wakili wake anasema Marekani haina mamlaka ya kumsafirisha kutoka Dubai.

“Kwa maoni yangu, FBI na serikali hapa walivunja sheria walipo mtekanyara kutoka Dubai bila mchakato wowote wa kisheria unaowaruhusu kufanya hivyo ,” Bwana Pissetzky toaliiambia BBC.

“Hapakua na mchakati wa kisheria wa kumsafirisha, hapakua na nyaraka za kisheria zilizowasilishwa, likua ni wito wa FBI. Sio raia wa Marekani, Marekani haina kabisa mamlaka ya kumchukua ,” alisema wakili wake.

Lakini polisi ya Dubai ilisema katika ujumbe wake wa Facebook kwamba mkurugenzi wa FBI aliwashukuru kwa kuwasafieisha wanaume hao wawili.

Presentational grey line

Anashutumiwa kwa kosa gani?

Ray Hushpuppi tayari ni mtu maarufu sana kwenye Instagram kwa maisha ya kifahari (kula bata) ambayo aliyanadi kupitia picha alizozituma kwenye mtandao huo , lakini alipata ufuasi zaidi wa watu 100,000 baada ya kukamatwa kwake.

Alipokamatwa polisi ya Dubai ilisema kuwa imepata dola milioni 40 taslimu , magari 13 ya kifahari yenye thamani ya dola milioni 6.8, kompyuta 21, simu 47 za smartphone na anwani za watu karibu milioni mbili wanaodaiwa kuwa waathiriwa wa wizi wake .

Glen Donath aliyekua mwendesha mashtaka zamani mjini Washington anasema wanaume hawa “walizidi kujidai kwani walijinadi kupita kiasi katika mitandao ya kijamii “.

Ruka Instagram ujumbe, 1

Mwisho wa Instagram ujumbe, 1

Transparent line

Taarifa hii iliwashangaza wengi ambao wamekua wakifuatilia maisha yao ya hali ya juu kwenye mitandao ya kijamii, wakijiuliza wanaume hawa wanatoa wapi pesa kiasi hicho.

Bila kujua walichokua wakikifanya, kwa kuonesha maisha yao ya hali ya juu katika mitandao wa Instagram na Snapchat, wanaume hawa walikua wakitoa utambulisho wao kwa majasusi wa Marekani.

Kwa sasa, wanashtakiwa kwa kudanganya kuwa ni wafanyakazi wa kampuni mbalimbali nchini Marekani , kuandika barua pepe wakiwadanganya watu ambao waliwatumia mamilioni ya dola kwenye akaunti zao.

Katika mtandao wa Instagram , “hushpuppi” anajitambulisha kama mtaalamu wa ujenzi, na hata kuna picha zinazoonesha nyumba anayoijenga. Lakini ”nyumba” hizo alizitumia kama njia ya ulaghai na wizi, kulingana na wapelelezi.

“Mfumo wetu wa maadili yetu ya Nigeria inapaswa kuangaliwa, hususan thamani tunayoipatia mali, kwa vyovyote vile unavyoipata . Ebuka Emebinah,mtaalamu wa masuala ya uchumi .” ameiambia BBC .

”Ni utamaduni ambapo watu wanaamini kwamba matokeo yanakuelezea . Hatuweki msisitizo katika mchakato na hili limejengwa kwa muda”

Ruka Instagram ujumbe, 2

Mwisho wa Instagram ujumbe, 2

Walilenga timu ya ligi ya Primia.

Mwezi Aprili , “hushpuppi” alibadilisha upya makubaliano ya kukodi nyumba ya kifahari sana Dubai kwa majina yake halisi na simu yake binafsi.

Wiki mbili kabla ya kutiwa nguvuni, aliweka picha yake kwenye Instagram akiwa karibu na magari yake mawili ya Rolls-Royce akaandika ujumbe:

“Asante Mungu, kwa Baraka nyingi maishani mwangu. Endelea kuwaaibisha wale wanaosubiri niaibike”

“Maisha ya kifahari ya Abbas yanatokana na uhalifu, pia ni mmoja wa watu wanaoongoza kwa wizi wa mtandao kwa kuvamia kompyuta za watu, wizi wa pesa kwa njia ya ulaghai wakiwalenga watu kote duniani katika mfumo uliotengenezwa kwa lengo la kuwaibia mamilioni ya dola “. Ilisema taarifa ya Shirika la upelelezi la Marekani FBI kuhusu uchunguzi.

Katika kisa kimoja, kampuni ya fedha inasema iliibiwa dola $14.7 kwa njia ya mtandao, inasema kuwa fedha hizo zilikwenda kwenye akaunti za “hushpuppi” zilizpo katika nchi mbali mbali duniani.

Waraka wa mashtaka unaonyesha kuwa mtu huyo anakabiliwa na shitaka la la kuiba dola milioni $124 kutoka kwa moja ya timu ambayo haikutajwa ya Primia Ligi.

FBI limesema kuwa lilipata taarifa katika mitndao Google, Apple iCloud, Instagram na Snapchat, akaunti za benki , stakabadhi zake za usafiri, mawasiliano na washirika wake katika wizi na rekodi za utumaji wake wa pesa.

mrwoodbery in front of Lamborghini

‘Yahoo boys’

Takriban 90% ya barua pepe za utapeli hutoka Afrika ya magharibi kulingana na taasisi ya Marekani ya usalama wa kimtandao , Agari.

Crane Hassold anayeshughulikia uhalifu wa aina hii katika taasisi Agari. Anasema: ”Wanaofanya utapeli huu huanza kwa kuchunguza barua pepe za mawasiliano halisi katika kampuni fulani zinazofanya biasharana kuchukua anwani za barua pepe zao na baadae kupotosha mawasiliano hayo kwa kusema kuwa walibadili akaunti za benki za malipo na kuwaomba waanze kutumia akaunti hizo mpya kwa malipo”.

Bwana Ponle ambaye anatumia jina la “mrwoodberry” katika mitandao ya kijamii, alitumia jina la Mark Kain katika barua pepe” ilisema FBI.

Anashutumiwa kuilaghai kampuni ya mjini Chicago iliyomtumia dola milioni $15.2.

Na kampuni nyingine za Iowa, Kansas, Michigan, New York na California pia zinasema kuwa ziliathiriwa na utapeli huo.

Pesa hizo baadae zilipotea kwani baada ya kutumwa kwa pesa hizo zilibadilishwa kuwa pesa mbadala zinazotumiwa kwa njia ya mtandao zinazofahamika kama ‘cryptocurrency bitcoin’.

Wizi wa aina hii unaofanyika kwa njia ya barua pepe umeshamiri sana duniani na kwa kiwango kikubwa unahusishwa na Nigeria na kwamba nyota wa wizi huo Nigeria wanaitwa ‘Yahoo boys’.

FBI inawatahadharisha watu wawe makini wanapofanya mawasiliano ya barua pepe zinazowahakikishia kuwa watapata pesa nyingi au wale wanaowaambia wabadili njia yao ya kawalida ya malipo.

Mwandishi wa BBC aliandikiwa hivi karibuni ujumbe ambao ulikua karibu sawa na ule unaoelezewa katika taarifa hii.

Presentational grey line

Jinsi wizi unaofahamika kama 419 na mapenzi unavyofanya kazi

Romance scam

•Mtu hukuandikia baruapepe, akikuambia kuwa anataka umsaidie kutuma pesa

•Atakwambia kuwa matatizo ya kisiasa au matatizo ya majanga mengine vinamzuwia kutuma pesa

•Atakuomba umpe akaunti yako ili atume pesa

•Hii humsaidia kuifikia akaunti yako na kuweza kuondoa pesa

s

Wakili Moe Adele, mwenye makao yake mjini Washington, anasema inasikitisha kwamba serikali ya Nigeria haijali matatizo ya vijana Wanigeria wanaojiingiza katika vitendo vya aina hii.

“Wanaviona vitendo hivi kama njia rahisi kuwasaidia katika nchi inayowapatia fursa chache na wakati mwingine haipo.”

Ayo Bankole -muasisi mwenza wa Bootcamp yenye makao yake nchini Nigeria anasema: ”Kuna Wanigeria wengi wanaofanya mambo mengi mazuri duniani, lakini wanaofanya mabaya huchafua sura ya nchi.

“Kampuni nyingi siku hizi hazitumi bidhaa nchini Nigeria, kampuni nyingi hazikubali malipo kutoka imetuharibia sura .”

Katika ripoti ya mwaka 2019 kuhusu uhalifu wa kimtandao , FBI ilisema kuwa ilipokea malalamiko karibu 460,000 ya visa vinavyoshukiwa kuwa ni wizi wa kumtandao, huku zikibiwa dola bilioni $3.5 na zaidi ya dola $300 ziliweza kurejeshwa.

Hatahivyo, wengi miongoni mwa wahusika wa wizi huu hawakamatwi, na ni wachache wanofika jela kwani wizi huu huvuka mipaka na hutekelezwa kwa njia ngumu, kulingana na Glen Donath

Iwapo watapatikana na hatia Ibyaha, Bwana Abbas na Bwana Ponle wanaweza kufungwa kifungo cha miaka 20 jela.

Chanzo BBC.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents