Habari

Wakufunzi kutoka (WHWB) kuwajengea uwezo wakaguzi wa OSHA na WCF, DC  Mwaisumbe atoa neno (+Video)

Mkuu wa Wilaya ya Longido Mhe Frank Mwaisumbe amewapongeza OSHA  kwa kubadili mfumo wa utendeji kazi kwa kuondoa urasimu wa utendaji kazi, kwani hupelekea shughuli nyingi kukwama, na hivyo wawekezaji wengi kukimbia nchini kuwekeza.

Mkuu huyo wa Wilaya ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa  Arusha Mhe Mrisho Gambo, amesema hayo leo jijini Arusha wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo kwa wakaguzi wa Afya toka OSHA na WCF, na kuongeza kuwa juhudi za kupunguza TOZO kutasaidia OSHA kuweza kuwafikia wawekezaji wengi zaidi na hivyo suala la Usalama na Afya Mahali Pa kazi kuanza kutekelezwa  na waajiri wengi.

Awali akimkaribisha Mkuu wa Wilaya, Kaimu mtendaji mkuu wa OSHA, Bi Khadija Mwenda amesema mafunzo hayo yameandaliwa kwa lengo la kuwaongezea uwezo watumishi wa Umma ili kutoa huduma bora katika maeneo yao ya kazi.

Naye mjumbe wa shirika la Workplace Health without Borders kwa Upande wa Tanzania,  amesema lengo kubwa la taasisi hiyo ni kuhakikisha inatoa mafunzo yanayolenga kuondoa changamoto za usalama na Afya Mahali Pa kazi duniani.

Mafunzo haya ya wiki moja yameandaliwa na OSHA kwa lengo la kuwajengea uwezo wa wakaguzi wa OSHA pamoja na WCF, na yanaendeshwa na wakufunzi wa Canada, Marekani na Ubelgiji kutoka shirika la kimataifa la Workplace health without Border (WHWB).

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents