Habari

Walemavu 350 wajitokeza kupokea miguu ya bandia kwa RC Makonda

Zaidi ya walemavu 350 wamejitokeza katika zoezi la upimaji miguu ili kupatiwa miguu ya bandia itakayowasaidia kufanya shughuli zao kirahisi.

RC Makonda akiwa na walemavu hao

Zoezi hilo limeandaliwa na mkuu wa mkoa wa Dar es saaam Paul Makonda ikiwa ni juhudi za kuwasaidia wananchi wa mkoa wake, ili kupambana vema katika ujenzi wa taifa.

“Ni wajibu wa serikali kusaidia kupunguza makali mnayoyapitia, maana kuna wengine baadhi yenu hawana uwezo wa kununua miguu hii ya bandia,na wengine ndugu zao wamewatelekeza baada ya kupatwa na ulemavu, na ndo maana niliweza kuwatafuta wadau watakao weza kuniunga mkono na hatimae wakawa na moyo katika kuniunga mkono kuwasaidia nyinyi wananchi wangu”Makonda alisema.

Makonda amesema yote hayo anayafanya kwa mujibu wa Rais John Pombe Magufuli ambae amempa nafasi ya kuiongoza Dar es salaam, hivyo analazimika kufanya kazi kwa jitihada zote kuhakikisha wananchi wote wanapata huduma inayostahiki.

Aidha ameeleza kuwa miguu hiyo haitolewi bila ya mlemavu kupimwa, ambapo itawasaidia wataalamu kujua aina ya tatizo walio nalo.

“Inasaidia Kujua saizi ya mguu, wapi umekatikia,waweze kujua wapi uonganishwe na wapi hauwezi kuunganishwa, na wakati mwengine wanahitaji kujua historia ya tatizo lako ili kukupatia kitu ambacho hakitakuletea tatizo tena hapo baadae, na ukipewa mguu bila kupimwa unaweza kupewamguu ambao baada siku mbili au tatu unageuka kuwa tatizo, Alisema Makonda.

Zoezi hilo halikuweza kuhudhuliwa na wananchi walemavu wa mkoa wa Dar es salaam pekee, Bali na wengine kutoka mikoa mbalimbali nchini ikiwamo Pwani,Tanga,Morogoro,Songea, ambapo wengiwao walilazimika kulala nje za ofisi za Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam zilizo ilala Jijini humo.

Makondaameeleza hali hiyo ni sahihi kwa kutokana yeye habagui na wote wanatumika chini ya mwamvuli wa Rais John Pombe Magufuli ambae ni Rais wa watanzania wote, ambapo amewahakikishia wote kupata huduma inayo stahiki.

Idadi ilikuwa ikitarajiwa ni ya watu mia mbili lakini hali ambayo imeleta changamoto ya idadi kubwa ya watu kuliko ile iliyopangwa.

Kwa upande wa Mganga mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Dr. Grace Magembe ameelezaea takwimu za ajali zitokeazo katika mkoa wake ni takribani mia nane ,mpaka eflu moja na atika hao asilimia 40% mpaka 45% wanapoteza viungo vyao vya mwili ikiwamo mikono,miguu, vidole.

Naye Dr.Grace Magembe. Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari kuhusiana na zoezi la hilo.leo jijini Dar es salaam.

“Nawaomba sana wananchi tuweni makini sana barabarani,Madereva wa
magari,bodaboda,Maguta,Baiskeli ,watembea kwa miguu tufate taratibu za usalama barabarani watu wote hawa asilimia kubwa ulemavu wao ni unatokana na ajali, kuna usemi usemao watu wa Dar es salaam ni wajanja wa mjini ,wanaogopa mvua kulio gari watu wakiona mvua wakimbia sana kuliko gari kwa hiyo tusilete masihara kwenye vitu kama hivi”. Alisema Dr. Grace

Nao baadhi ya walemavu wametoa shukrani zao za dhati kwa Rais Magufuli kupitia mkuu wao wa mkoa Mkoa wa Dar es alaam Paul Makonda kwa kuwajali, na kusema kwa hatua hiyo hawana cha kumlipa Mkuu wao isipokuwa ni Mungu pekee ndie atakae walipa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents