Habari

Walimu kuendelea kupatiwa mafunzo maalum- Mh. Manyanya

By  | 

Serikali kupitia Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia imesema imeandaa mtaala mpya ambao umeandaliwa katika misingi ya elimu jumuishi ambao ulianza kutumika kuanzia mwaka wa masomo 2014/2015 ili kumudu wanafunzi wenye mahitaji maalum.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Mhe.Eng,Stella Manyanya wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Mhe.Stella Ikupa Alex aliyetaka kujua Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha kila mwalimu anapatiwa mafunzo maalum yatakayomwezesha kufundisha wanafunzi wenye ulemavu.

“Hadi sasa wahitimu wa ngazi ya Stashahada ya Elimu maalum wapatao 158 wamehitimu Octoba 2016 na wanachuo 248 wanaendelea na masomo katika chuo cha Ualimu Patandi”,Aliongeza Mhe.Manyanya.

Aidha Waziri uyo amesema kuwa kutokana na umuhimu wa walimu hawa Wizara yake katika mwaka wa fedha 2016/17 iliendesha Mafunzo kwa walimu 519 walio kazini wanaofundisha darasa la kwanza na la pili kuhusiana na mtaala ulioboreshwa ili kumudu ufundishaji wa wanafunzi wenye mahitaji maalum.

Pamoja na hayo tarehe 20 mpaka 28 Juni,2017 walimu 712 walio kazini wanaofundisha wanafunzi wenye ulemavu wa akili na wenye usonjo walipatiwa mafunzo katika vituo vya Mwanza,Arusha,Mbeya na Morogoro ili kuwajengea uwezo wa kumudu ufundishaji wa wanafunzi wenye ulemavu huo.

“Walimu 600 wanaofundisha darasa la tatu na nne watapatiwa mafunzo ya Mtaala ulioboreshwa kuanzia tarehe 10 hadi 30 Julai,2017 lengo ni kuwafikia wengi zaidi”Alisisitiza Mhe.Manyanya.

Na Laila Sued

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments