Habari

Walimu waliokuwa wanafanya kazi chini ya mti wakabidhiwa ofisi na RC Makonda (Video)

Kilio cha muda mrefu cha walimu wa shule ya msingi Vijibweni Wilaya ya Kigamboni kufanya kazi chini ya Miti, kwenye vikorido,kwenye madawati na kujisaidia kwa majirani kutokana na ukosefu wa ofisi ya walimu leo kimepatiwa ufumbuzi baada ya Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda kuwapatia ofisi ya kisasa yenye hadhi ya kimataifa.

Ofisi hiyo ya kisasa aliyokabidhi RC Makonda ujenzi wake umegharimu zaidi ya Shilingi Milioni 200 ambapo ndani yake ina ukumbi mikutano, Ofisi ya mwalimu mkuu, Mwalimu mkuu msaidizi,ofisi ya walimu wote, Chumba cha kuhifadhi mitihani, stoo, sehemu ya mapokezi, chumba cha kubadilishia nguo, vyoo vya kisasa na bafu huku ikiwa imefungwa viyoyozi (AC) ili kuhakikisha walimu wanafanya kazi kwa uhuru.

Akizindua ofisi hizo RC Makonda amesema dhamira yake ya kuhakikisha walimu wanafanya kazi katika mazingira bora ipo palepale kwakuwa anatambua thamani ya mwalimu ni kubwa kwenye jamii hivyo wanastahili kupewa heshima.

Aidha RC Makonda ameishukuru Kampuni ya CRJE East Afrika ya nchini China iliyoamua kumuunga mkono kwa kujenga ofisi mbili za walimu kwa lengo la kuwawezesha walimu kufanya kazi katika mazingira mazuri.

Kwa upande wao walimu wa Shule ya Vijibweni kwanza wamemshukuru RC Makonda kwa kuwajengea ofisi hiyo ya kisasa kwakuwa awali walikuwa wakifanya kazi katika mazingira magumu ikiwemo chini ya miti na wamekuwa wakitumia choo kimoja na wanafunzi na wakati mwingine kujisaidia kwa majirani wens.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents