Siasa

Walioenguliwa CCM kujipanga 2010

Wana CCM waliopanguswa katika chaguzi zilizopita ndani ya chama hicho wakiwemo baadhi ya majeruhi wa ‘ajali za kisiasa’ zilizotokea hivi karibuni wanadaiwa kuanza mkakati wa kujiweka sawa na kujipanga upya ndani na nje ya chama hicho

Wana CCM waliopanguswa katika chaguzi zilizopita ndani ya chama hicho wakiwemo baadhi ya majeruhi wa ‘ajali za kisiasa’ zilizotokea hivi karibuni wanadaiwa kuanza mkakati wa kujiweka sawa na kujipanga upya ndani na nje ya chama hicho kwa ajili ya uchaguzi mkuu ujao mwaka 2010.

 
Mkakati wa kwanza unaodaiwa kufanywa na makundi hayo ni kuwatumia viongozi wa serikali na makada walioko ndani ya chama katika ngazi za wilaya na mikoa kuwajengea mtandao imara wenye nguvu utakaotoa msukumo wa kushinda ndani ya vikao vya uteuzi wa chama hicho.

 
Uchunguzi umebaini kuwa kundi la kwanza ni lile la wana CCM walioachwa baada ya uchaguzi mkuu wa chama hicho Novemba 2007 na lingine ni la wanachama waliokumbwa na dhoruba na kuachia nyadhifa zao serikalini baada ya kuhusishwa kwa njia moja ama nyingine na kashfa zilizoibuka hivi karibuni.

 
Imedaiwa kuwa pilika hizo zimeanza kupamba moto baada ya kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC) kilichofanyika kijijini Butiama mkoani Mara ambapo watendaji kadhaa wa chama ngazi za mikoa na wilaya, wamehamishwa kwa madai ya kuziba nafasi na kuleta ufanisi wa utendaji katika mikoa na wilaya husika.

 

 

 

Sambamba na hilo mpango mwingine ulioandaliwa ni kuwaingiza kwenye mtandao huo makada wenye ushawishi mkubwa kufuatilia nyendo za wanachama wenzao wanaoonekana kumuunga mkono Mwenyekiti wa chama hicho Rais Jakaya Kikwete katika msimamo wake wa kuwawajibisha wanachama wanaokumbwa na kashfa mbalimbali ndani ya chama na serikalini.

 

 

 

Vyanzo vyetu vilidokeza kwamba ‘wanaosajiliwa’ kwenye kundi hilo wamekuwa wakipewa ahadi mbalimbali zikiwemo fedha na vitendea kazi vikiwemo vinasa sauti ili kukusanya taarifa mbalimbali kutoka kwa watu wenye misimamo tofauti ili zitumike baadaye kuandaa mikakati ya kudhibiti mambo yanayoweza kukwamisha malengo yao.

 

 

 

Ili kuhakikisha kundi hilo linajipanga vyema, inadaiwa kuna harakati za siri ‘kuwabomoa’ kisiasa viongozi wanaoonekana kuwa na uwezo mkubwa wa kudhibiti ufisadi.

 

 

 

Katika kutekeleza hilo hivi karibuni kundi hilo linadaiwa kuandaa mkakati maalum kuzua uvumi kwamba kuna baadhi ya viongozi wastaafu wa chama na serikali wanafanya vikao vya siri na baadhi ya majeruhi wa kisiasa ili kuwaharibia uhusiano viongozi hao na Chama Cha Mapinduzi. chaguzi mkuu ujao mwaka 2010.

 

 

 

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents