Habari

Waliofariki katika ajali ya moto California yafikia 71, zaidi ya 1000 hawajulikani walipo (Picha)

Idadi ya Watu waliofariki kutokana na ajali ya moto unaochoma msitu nchini Marekani imefikia 71 huku zaidi ya watu 1,011 hawajulikani walipo, Askari Kory Honea amesema hayo jana Novemba 16

Zimamoto wamejikuta wakipambana na aina mbili za moto katika msitu huo ambapo awali walikuwa walipambana na moto uliopewa jina la ‘Camp Fire’ uliopo katika Kaunti ya Butt lakini sasa umeibuka mwingine katika Kaunti ya Ventura uliopewa jina la ‘Woolsey Fire’

Wameeleza kuwa Mvua ingezaidia kuuzima moto huo lakini ingeleta ugumu katika kuwatafuta waliopotea na kupoteza maisha kutokana na kwamba wamekuwa wakikutana na mifupa tu au vipande vya mifupa ya watu.

Camp Fire umeharibu nyumba 9,700 na majengo 144 na hadi kufikia jana ulikuwa umezimwa kwa 45% na sehemu iliyobaki haihatarishi maeneo yenye watu wengi

Aidha, Kusini mwa California watu zaidi wamekuwa wakiruhusiwa kurudi majumbani kwao baada ya asilimia 69 ya Woolsey Fire kuzimwa hadi kufikia jana usiku, moto huo umeteketeza nyumba 600.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents