Habari

Waliohusika na shambulio la London watambulika

Jeshi la polisi la nchini Uingereza limefanikiwa kuwatambua watu wawili kati ya watatu waliofanya shambulio huko London Bridge siku ya Jumamosi.

Watu hao walisababisha vifo vya watu saba na wengine 48 walijeruhiwa katika shambulio hilo lakini baadaye na wao waliuawa kwa kupigwa risasi.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la CNN, limesema waliohusika na tukio hilo ni Rachid Redouane 30, na Khuram Shazad Butt 27. Wakati huo huo kundi la Islamic State lilitangaza kuhusika na shambulio hilo.

Hata hivyo Polisi wameweza kuwaachia huru watu wapatao 12 ambao waliwashikilia kwa tuhuma za kuhusika na shambulio hilo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents