Michezo

Waliokamatwa Mwanza walikuwa katika kampeni – TFF (Video)

Kamati ya uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) limejiridhisha kuwa wote waliokamatwa na TAKUKURU mkoani Mwanza walikuwa katika kampeni ya uchaguzi na hivyo imewaondoa wagombea hao katika kinyanganyiro hicho.

Bongo5 imemtafuta Afisa Habari na Mawasiliano wa Shirikisho la soka nchini, Alfred Lucas ili kuthibitisha taarifa hizo.

Afisa Habari na Mawasiliano wa Shirikisho la soka nchini, Alfred Lucas

“Kulikuwa na kamati ya uchaguzi  ambayo  kati ya moja ya ajenda zake ilikuwa ni kupitia majibu kutoka TAKUKURU nakuona kwamba je habari ya Mwanza ilikuwa vipi”.

“Pamoja na mambo mengine waliyoandika lakini kubwa ni kwamba ilijiridhisha kamati ya uchaguzi kwamba wale waliyokamatwa Mwanza walikuwa katika kampeni na kwa kufanya hivyo ni kuvunja sheria kanuni ya 14 kipengele cha tatu inazuiwa mapema”.

“Kampeni zitatangazwa tu pale watakapo ruhusiwa na kwa msingi huo adhabu ya kikanuni ni kuwaondoa

kwenyekinyang’anyiro ama mchakato lakini bado wanahaki kwa msingi huo wanaweza kukata rufaa”.

Shaffih Dauda akiri kufanyiwa mchezo mchafu

Siku ya Jumatano ya July 26 2017 zilienea taarifa za kukamatwa na TAKUKURU baadhi ya wadau wa soka wakiwemo wagombea wa uchaguzi katika nafasi mbalimbali za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

Shaffih Dauda ajiengua uchaguzi TFF

Miongoni mwa hao ni Mwenyekiti wa Chama cha Mpira Dar es Salaam (DRFA) Almas Kasongo, mgombea wa nafasi ya ujumbe wa kamati ya utendaji ya TFF kanda ya Dar es Salaam na mchambuzi wa habari za michezo Tanzania Shaffih Dauda pamoja na wanafamilia wengine wa mpira Mwanza.

By Hamza Fumo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents