Habari

Waliokuwa katika mashindano ya roboti Marekani wapotea

By  | 

Vijana sita kutoka nchini Burundi, waliokuwa wakishiriki katika mashindano ya roboti nchini Marekani wameripotiwa kutoroka katika mashindano hayo.

Baada ya msimamizi wa timu hiyo kushindwa kuwapata vijana hao walio na umri kati ya 16 hadi 18, ndipo aliamua kuripoti kuto waoana. Wakiwemo wanaume wanne na wanawake wawili, majina yao ni Don Ingabire, Kevin Sambukiza, Nice Munezero, Audry Mwamikazi, Richard Irakoze na Aristide Irambona.

Idara ya polisi mjini Washington DC, imesema kuwa mara ya mwisho vijana hao kuonekana ilikuwa siku ya Jumanne wakati wa makamilisho ya mashindano, pia inadaiwa kuwa vijana wawili kati yao tayari wamevuka mpaka na kuingia Canada lakini bado haijathibitishwa na polisi.

Na Laila Sued

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments