Waliyozipiga NBA waadhibiwa

Chama cha Taifa cha Mpira wa Kikapu nchini Marekani (NBA) kimewasimamisha mchezo mmoja mshambuliaji wa timu ya Miami Heat, James Johnson na Serge Ibaka anayekipiga Toronto Raptors kwa kosa la kutaka kupigana usiku wa Jumanne wakati timu zao zilipokuwa zinacheza huko Toronto.

Majira ya saa 7:50 usiku nchini Marekani, robo ya tatu ya mchezo huo wachezaji, Ibaka na Johnson walivamiana na kuanza kusukumana wakati wakisubiria mpira .

Kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter, Johnson amewaomba radhi wachezaji wake, benchi zima laufundi, NBA na mashabiki wake kwakitendo kilichotokea katika mchezo huo.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW