Burudani

Walter Chilambo wa gospel ni hatari ya ulivyokuwa ukimjua

Ni swali ambalo wengi hujiuliza na wasipate majibu ya kuridhisha, kwamba kwanini washindi wa Bongo Star Search huwa hawafanikiwi? Inashangaza sababu uwezo wao wawapo kwenye shindano hilo huwa mara mbili zaidi ya wasanii maarufu wanaofanya vizuri, lakini wakishaingia tu mtaani hushindwa kufanya muziki wa maana.

201d33a1-f8f9-4b5a-a4d1-107e7ee09d30

Licha ya kuwa mmoja wa waimbaji bora kuwahi kutokea, Walter Chilambo aliyeshinda shindano hilo mwaka 2012, naye alijikuta akisombwa na upepo huo. Ilifikia wakati Walter aliacha kuachia nyimbo mpya na kufanya tu cover hali iliyowafanya baadhi ya watu kudhani kuwa ameishiwa.

Kumbe muimbaji huyu kutoka Mbeya alikuwa ni kama kobe aliyeinama akitunga sheria na kutafakari njia nzuri ya kurejea kuonesha uwezo wake. Ukimya wake ulimsaidia kuutambua muziki anaoweza kufanya na kupata heshima anayostahili.

Walter ameamua kuimba muziki wa injili na kwa wimbo wake Asante, ni dhahiri amedhamiria kuja kuokota kila senti aliyopaswa kuikota tangu kitambo. Asante ni wimbo unaotoa tafsiri ya muziki wa injili wa kisasa. Ni wimbo mtamu, wenye hisia na utunzi unaoweza kukutoa vinyweleo vya baridi kwa msisimko.

Ni utunzi wa aina yake unaofungua ukurasa mpya wenye kila dalili ya mafanikio makubwa. Asante ina video safi inayoendana na ukubwa wimbo wake na kwa waumini wa dini ya kikristo wimbo huu una nafasi ya kuwa maarufu kwenye playlist zao.

Sasa muimbaji huyo anajiweka kwenye ligi moja na Gudluck Gosbert – muimbaji mwingine mahiri wa gospel ya kisasa. Anaongeza idadi ya waimbaji wa muziki wa injili wanaoweza kuipa Tanzania sifa nyingine kama ambavyo wasanii kama Diamond, Alikiba, Vanessa Mdee na wengine wanaipa katika muziki wa Bongo Flava.

Kwa alichokifanya Walter ni kama kujivua gamba na kurudi upya katika muziki ambao kwa sasa si kama huduma tu, bali biashara kama tu muziki wa kidunia ulivyo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents