Burudani

Wamarekani wachukizwa na kitendo cha Chris Brown kuvaa kama Taliban kwenye Halloween party ya Rihanna

Chris Brown (katikati) akiwa na washkaji zake

Juzi Rihanna aliandaa party ya Halloween huko West Hollywood na kukaribisha mastaa kibao akiwemo swahiba wake Chris Brown.

Chris ndiye aliyezua mjadala kutokana na kuvaa kama wanamgambo wa Taliban. Akiwa amevaa nguo hizo Chris alivaa pia mkanda wa risasi kifuani mwake pamoja na kushikilia machine gun huku akipewa kampani na washkaji zake waliokuwa wamevaa kama yeye.

Aliweka picha hiyo kwenye mtandao wa Instagram na kuandika “Ain’t nobody F**king wit my clique!!!!”

Mastaa wengine waliohudhuria party hiyo ni pamoja na Flo Rida, Paris Hilton, na staa wa Olympic Lindsay Vonn.

Baada ya watu kumshambulia Chris kwa kitendo hicho cha kuwaunga mkono magaidi mama yake Joyce Hawkins alimtetea mwanae kwa kuandika, “HALLOWEEN IS FOR FUN NOTHING MORE THAN JUST FUN. GET A LIFE PLEASE.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents