Wambura Aruhusiwa Kugombea

Baada ya kuipa shida kamati ya rufaa ya Shirikisho la Soka (TFF) wakati lilipojadili suala lake kuanzia alasiri hadi jana usiku, hatimaye Katibu mkuu wazamani Michael wambura ameruhusiwa kuingia kwenye kinyanganyiro cha nafasi ya makamu wa Rais

 

Baada ya kuipa shida kamati ya rufaa ya Shirikisho la Soka (TFF) wakati lilipojadili suala lake kuanzia alasiri hadi jana usiku, hatimaye Katibu mkuu wazamani Michael wambura ameruhusiwa kuingia kwenye kinyanganyiro cha nafasi ya makamu wa Rais
Wambura, ambaye anawania nafasi ya makamu wa kwanza wa rais wa TFF, alizuiwa kugombea nafasi hiyo baada ya kuwekewa pingamizi linalohusu fedha zilizotoka Shirikisho la Kimataifa la Soka (Fifa) na madai kuwa aliipa kampuni yake zabuni ya kufanya za shirikisho hilo.
Hata hivyo, Wambura alikata rufaa kwa kamati hiyo kupinga uamuzi wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF ya kumuengua kwenye kinyang’anyiro hicho, na jana ilikuwa siku ya tatu kwa suala lake kujadiliwa baada ya kuwasilisha vielelezo vyake.
Wafurukutwa wanaomuunga mkono mgombea huyo jana walikuwa wakihaha hadi usiku kwenye maeneo ya majengo ya ofisi za TFF wakitaka kujua hatma ya rufaa ya Wambura, ambaye naye alionyesha kuchukizwa na kitendo cha rufaa yake kutotolewa majibnu mapema.
“Nashangaa kwamba hadi saa hizi hawataki kutoa jibu la rufaa yangu,” alisema Wambura ambaye alikuwa ni miongoni mwa watu waliokuwa wakisubiri matokeo ya rufaa hiyo.
Mgombea huyo, ambaye pia ameingia kwenye malumbano na wanaoweza kuwa chini yake iwapo atashinda rufaa na uchaguzi akidai kuwa kumhujumu, jana jioni alitumia zaidi ya dakika 45 kuwakilisha utetezi wake kwa kamati hiyo ya rufaa iliyoanza kusikiliza utetezi wake kuanzia majira ya saa 11:00 jioni.
Wambura hakuonekana kutetereka baada ya kumaliza kuhojiwa na kamati hiyo, huku wengi wakijiuliza sababu za kuchukua muda mrefu kuhojiwa.
Baada ya Wambura kutoka kwenye chumba cha kamati hiyo, mawakili wake wawili waliingia kwenye jopo hilo lililokuwa chini ya Jaji John Mkwawa. Mawakili hao pia walitumia muda mwingi kuwakilisha hoja zao.
Wakati huo huo, wajumbe wa mkutano mkuu wanataraji kuwasili jijini Dar es salaam kuanzia leo na mwenyekiti wa Chama cha Soka cha Dar es salaam (DRFA), Amir Bharesa alisema wamejiandaa vizuri kwa uchaguzi huo utakaofanyika keshokutwa.
Alisema jumla ya wajumbe 116 wanatarajia kushiriki katika mkutano huo na baadaye katika uchaguzi utakaofanyika kesho kutwa kwenye ukumbi wa Water Front jijini Dar

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents