Habari

Wanafunzi 11 waliofanya ngono na mbwa Arusha hawatoshtakiwa

Wanafunzi wa kiume 11 wa shule za msingi Sombetini, jijini Arusha, wametuhumiwa kufanya ngono na mbwa eneo la mto Ngarenaro. Watoto hao ni wa miaka kati ya miaka saba na 11 na wanasoma darasa la tatu.

mbaroni

Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo amesema jeshi la polisi haliwezi kuwafungulia kesi wanafunzi hao ambao wamekiri kufanya vitendo hivyo mara kadhaa, kutokana na umri wao kuwa mdogo.

“Tukio hilo limetokea kuna watoto walikuwa wanafanya mapenzi na mbwa. Taarifa baada ya kupokelewa tulienda kuwapata hao watoto na katika kuwahoji tuligundua kuwa ni watoto mchanganyiko wengine wana miaka 8 wengine 9 wengine 10 wengine 11, ni watoto wadogo ambao kisheria ni kwamba mtu kushtakiwa na hilo kosa la kuzini anapaswa angalau awe ni mtu mzima kuanzia miaka 13 na kuendelea. Moto wa miaka 10 kumi na kurudi nyuma, ni kwamba kisheria hastahili kushtakiwa kwa jambo lolote lile alilolitenda la kijinai na mtoto wa miaka 11 mpaka 12 ni lazima ujiridhishe kwamba wakati wanafanya kosa alikuwa na uelewa wa kutosha kwamba kosa hilo analolitenda ni kosa kwahiyo ni wengi ambao wako excluded na sheria,”alieleza.

“Lakini hata hivyo kwasababu ya tukio walilolifanya ni kinyume na maadili ya binadamu, jeshi la polisi pamoja na udogo wa umri wao, limeelekeza dawati la jinsia kufika hapo shuleni na kuwapa counselling na pia kuwapa elimu ya kutosha ili waweze kuondokana na fikra ambazo wameshazizoea,”aliongeza.

“Lakini hata hivyo tunafanya uchunguzi kubaini mtu aliyewawezesha hao watoto kufanya vitendo vichafu kama hivyo ili tuweze kumchukulia hatua za kisheria. Lakini watoto kama watoto tutawapa elimu kama elimu pamoja na kuwapa wazazi wao, walimu pamoja na wazazi waweze wanafuatilia nyenzo za watoto wao wanapokuwa shuleni ili kuhakikisha kwamba wanafuata yale maadili ambayo wanawafundisha.”

BY: EMMY MWAIPOPO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents