Wanafunzi kulazwa chali kutazama jua ikiwa ni adhabu

Wanafunzi zaidi ya 1,000 wa kwenye shule za msingi tatu tofauti zilizopo kwenye kata ya Uvinza wanalazimishwa kuwahi masomo usiku na wanaochelewa hulazwa chali kama moja ya adhabu

Wanafunzi zaidi ya 1,000 wa kwenye shule za msingi tatu tofauti zilizopo kwenye kata ya Uvinza wanalazimishwa kuwahi masomo usiku na wanaochelewa hulazwa chali kama moja ya adhabu.


 


Malalamiko hayo yalielezwa na baadhi ya wazazi na Mwenyekiti wa Kijiji cha Uvinza wakati wakizungumza na mwandishi kwa njia ya simu kuhusiana na mikasa hiyo ambayo huwakumba watoto wao na wanafunzi kwa ujumla.



Wakiiijadili hatua ya walimu hao kuwataka kufika shuleni saa 11 alfajiri na wanaochelewa kuwalaza wanafunzi kuangalia jua na kama moja ya adhabu ni hatari, “alisema tabia hiyo ya walimu hao kuwalazimisha watoto hao kulala chali wakiangalia jua kama moja ya adhabu ni hatari kwa watoto hao kwani wanaweza kuwasababishia maradhi makubwa sana” alisema mmoja wa wazazi walioonekana kumizwa na kitendo hicho.



Mzazi mwingine aliyejulikana kwa jina la, Bw. Alphonce Lugema, alieleza kuwa “mbali na kulazwa chali pia walimu hao wamekuwa wakiwataka wanafunzi hao kuwahi shule saa 11 alfajiri wakati muda unakuwa umefunikwa na giza lilaoweza kupelekea kuwa na hali flani ya hatari kwa watoto hao”.



Alipoulizwa kuhusu hali hiyo, Ofisa Tarafa ya Nguruka, Bw. Mikidadi Daudi, alikiri kupata taarifa hizo na kusema si uungwana kulaza watoto kuangalia jua na kuwataka kufika shuleni saa 11 alfajiri.


 


Alisema ofisi yake itachukua jukumu la kufuatilia ili kujua kiini cha matatizo hayo ambayo yanalalamikiwa sana na wazazi kwa watoto wao kufanyiwa vitendo vya kikatili na walimu hao wa shule hizo tatu.


 


 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents