Habari

Wanafunzi wakamatwa kwa kuhamasisha maandamano na kumkashfu Rais Magufuli

By  | 

Wanafunzi tisa wa Chuo Kikuu cha Stella Maris na Daktari wa Hospitali ya Mission Nanyamba wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara kwa tuhuma za kumkashifu Rais John Magufuli na kuhamasisha maandamano ya April 26.


Kamanda wa Polisi mkoani humo, Lucas Mkondya akizungumza na waandishi wa habari mwishoni mwa wiki alisema watuhumiwa hao kwa nyakati tofauti wamekuwa wakitumia mtandao wa kijamii wa WhatsApp na Telegram kumkashifu Rais na kuhamasisha maandamano hayo.

Kamanda Mkondya bila kutaja majina ya watuhumiwa hao kwa madai ya sababu za kiupelelezi, alisema daktari huyo ni kutoka Halmashauri ya mji wa Nanyamba.

“Ninatoa onyo watu wajiepusha kutumia mitandao ya kijamii vibaya na kusababisha uvunjifu wa sheria za nchi. Watuhumiwa wote tunawashikilia kwa upelelezi zaidi,” alisema.

Katika tukio lingine, Kamanda Mkondya alisema wanawashikilia wahamiaji haramu 23 waliokutwa katika nyumba ya kulala wageni eneo la Chikongola, Wilaya ya Mtwara.

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments