Habari

Wanafunzi watiwa rumande kwa kuandamana kupinga sheria mpya ya kutoza kodi kwenye mitandao ya kijamii

Wanafunzi wapatao watano wa Chuo Kikuu cha Makerere nchini Uganda wamejikuta mikononi mwa polisi baada ya kuandamana wakipinga sheria mpya ya mitandao ya kijamii inayowataka raia wote wa Uganda wanaotumia mitandao hiyo kutozwa kodi.

Mtandao wa gazeti la New Vision la nchini Uganda limeandika kuwa wanafunzi hao waliandamana juzi July 2, 208 ambapo walikuwa wanaandamana kuelekea bungeni jijini Kampala.

Uganda imepitisha rasmi sheria ya kutoza kodi kwa watumiaji wote wa mitandao ya kijamii, na sheria hiyo imeanza kufanya kazi Julai 01, 2018.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents