Habari

Wanakijiji wauwa mamba 300 kulipiza kisasi cha kijana wao

Wanakijiji wauwa mamba 300 kulipiza kisasi cha kijana wao

Wanakijiji magharibi mwa Papua nchini Indonesia wamewauwa takribani mamba 300 waliyokuwa wakipatikana kwenye sehemu ya hifadhi baada ya kijana mmoja kushambuliwa hadi kufa.

Picha kadhaa zimeenea kwenye mitandao ya kijamii zikionyesha wananchi hao wakiwa na silaha za jadi, mapanga, nyundo na visu baada ya kufanya tukio hilo la kulipiza kisasi.

Maafisa na polisi wanasema kuwa hawakuweza kuzuia mauaji hayo lakini watafungua mashtaka dhidi ya waliohusika.

Image result for West Papuan villagers slaughter hundreds of crocodiles after local

Kwa mujibu wa sheria za nchini Indonesia mtu yeyote anayekutwa na hatia ya kuuwa wanyama wanaopatikana kwenye hifadhi adhabu yake inaweza kuwa ni kifungo jela.

Kijana huyo alishambuliwa na mamba siku ya Ijumaa kisha kuzikwa Jumamosi ndipo wanakijiji hao wakaingia wenye hifadhi hiyo na kuwauwa mamba wote.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents