HabariMitindo

Wanamitindo wembamba wapigwa marufuku Ufaransa

Nchi ya ufaransa imeanza kutekeleza sheria inayopiga marufuku kuwatumia wanamitindo wembamba wasio na afya katika matangazo ya nguo au bidhaa..

Wizara ya afya ya nchini humo imasema kuwa, inataka kukabiliana na matatizo ya kutokula na viwango visivyofikiwa vya urembo. Hivyo basi wanamitindo hao watahitajika kuwa na cheti cha daktari kuonyesha afya yao kwa misingi ya vipimo vya uzito wao na kimo.

Mswada wa awali ulikuwa umependekeza uzito na kimo cha wanamitindo, hatua iliyopingwa na mashirika ya urembo nchini Ufaransa. Mnamo 2015 mswada mwingine uliungwa mkono na wabunge, pia ukiwaruhusu madaktari kuamua ikiwa mwanamitindo ni mwembamba mno kuambatanisha uzito wake na umri kubainika.

Kampuni za wanamitindo hao watapigwa faini ya hadi dola 82,00 au kifungo wakibainia kuwaajiri wanamitindo waliovunja sheria.Ufaransa sio nchi ya kwanza kuweka sheria inayohusu wanamitindo wembamba- Italia, Uhispania na Israel washafanya hivyo pia.

Na Laila Sued

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents