Habari

Wananchi 170 kufidiwa

Serikali itawafidia wananchi 170 ambao nyumba zao 32 zitabomolewa kupisha ujenzi wa kituo cha mabasi yaendayo kasi kitakachojengwa katika kata za Magomeni na Ndugumbi jijini Dar es Salaam.

Na Abdul Mitumba



Serikali itawafidia wananchi 170 ambao nyumba zao 32 zitabomolewa kupisha ujenzi wa kituo cha mabasi yaendayo kasi kitakachojengwa katika kata za Magomeni na Ndugumbi jijini Dar es Salaam.


Kwa mujibu wa taarifa ya Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), idadi hiyo ya watu inajumuisha wamiliki wa nyumba pamoja na wapangaji wao.


Ilisema nyumba zote ziko katika Manispaa ya Kinondoni na kwamba 19 zipo kata ya Magomeni na 13 zitakazovujwa zipo kata ya Ndugumbi.


Taarifa iliyotolewa na TAMISEMI kwenda kwa maofisa watendaji wa kata hizo inaonyesha kuwa kata ya Magomeni ndiyo itachangia eneo kubwa la ardhi kwa ajili ya ujenzi wa kituo hicho.


Katika taarifa hiyo majina ya wamiliki, namba za nyumba na viwanja vimetajwa lakini haikueleza kiasi cha fedha kitakachotumika kulipa fidia walengwa.


Kadhalika, taarifa hiyo hakusema zoezi la kuwalipa fidia wananchi litaanza lini ingawa mradi huo wa mabasi yaendayo kasi unatarajiwa kuanza ifikapo 2009.


Kituo hicho kitajengwa eneo la Magomeni Kota, jirani na ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni.


Wakizungumzia taarifa hiyo kwa nyakati tofauti, diwani wa kata ya Ndugumbi, Bw. Charles Mgonja na Ofisa Mtendaji wa kata ya Magomeni, Bi. Latifa Ramadhan, walisema wana imani malipo hayo yatatolewa mapema na bila usumbufu.


Awali kituo hicho ilikuwa kijengwe eneo la Kariakoo, katika kota zinazomilikuwa na wafanyakazi wa Bandari na TRA.


Lakini wafanyakazi hao waligomea mradi huo kwa madai kwamba wanao mradi wao wa kujenga maghorofa ya biashara katika eneo hilo.


Source: Nipashe

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents