Wananchi wenye hasira kali watibua ziara ya Rais Donald Trump nchini Uingereza (+picha)

Rais wa Marekani, Donald Trump jana Julai 12, 2018 alipokelewa kwa maandamano makali nchini Uingereza kwenye ziara ya kikazi ya siku nne nchini humo.

Image result for Trump in uk
Rais Trump akiwa na mkewe mapema jana baada ya kuwasili Uingereza

Maelfu ya raia wa Uingereza ambao walipinga ziara hiyo ya Rais Trump mapema mwaka huu, wamejitokeza kwenye maandamano hayo leo tena katika eneo viunga vya bunge la Uingereza na barabara kubwa jijini London wakiwa na mabango yenye ujumbe tofauti tofauti.

Image result for Trump UK Tour

Hata hivyo bado maandamano hayo hayajazuia chochote kwani Rais Trump leo anatarajiwa kuonana na Waziri Mkuu wa Uingereza, Bi. Theresa May na kesho akiwa na mkewe, Melania Trump watamtembelea Malkia Elizabeth.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW