Habari

Wanandoa wakabidhiwa jukumu la kusoma taarifa ya habari kwenye luninga wakiwa pamoja

Wanandoa wakabidhiwa jukumu la kusoma taarifa ya habari kwenye luninga wakiwa pamoja

Chombo cha habari cha Citizen nchini Kenya kimewatangaza wanandoa maarufu, Rashid Abdalla na mkewe Lulu Hassan kuanza kusoma taarifa ya habari wakiwa pamoja kila ifikao siku ya Jumamosi na Jumapili.

Rashid ambaye ni mume wa mwana dada Lulu alikuwa mtangazaji wa kituo cha NTV kabla ya kujiunga na Citizen ambapo amekabidhiwa majukumu hayo mapya akiwa sanjari na mkewe kwenye kipindi cha Nipashe Wikendi kinachoruka hewani kila Jumamosi na Jumapili kuanzia tarehe 21 mwezi Julai 2018.

Tukio hili la wanandoa kusoma habari wakiwa pamoja ni kwa mara ya kwanza linatokea nchini Kenya. Rashid Abdalla anachukua nafasi ya Kanze Dena ambaye aliajiriwa na Ikulu ya rais kuwa msemaji mnamo mwezi Juni.

Wakenya wengi wakisubiri kuona ikiwa wapenzi hao wataweza kufanya kazi kwenye osifi moja, huku uongozi wa Nipashe Wikendi wakithibitisha wawili hao kuanza kufanya kazi pamoja Julai 22, 2018.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents