Afya

Wanaochati na kuongea na simu chooni, Wapo hatarini kupatwa na gonjwa hili

Kama wewe ni kijana na umeathirika zaidi na matumizi ya simu kiasi kwamba hata chooni unaingia nayo ili uweze ku-chat au kuongea na simu, Basi acha tabia hiyo mara moja kwani itakugharimu kiafya.

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Daktari bingwa, Sarah Jarvis kutoka Uingereza, Umeonesha watu wengi wanaoingia na simu chooni na kuanza kuzitumia wamepatwa na ugonjwa wa Bawasiri.

Daktari huyo amesema kuwa kitaalamu, Chooni unatakiwa ujisaidie ndani ya dakika 5 na watu wengi wanaoingia na simu vyooni hutumia zaidi ya dakika 5 kujisaidia.

Sarah akiongea na gazeti la METRO, Amesema kitendo cha kukaa muda mrefu ukiwa unajisaidia haja kubwa husaidia bakteria kuzaliana na kuigia kuingia mwilini kwa urahisi.

Kwenye tafiti hiyo, Sarah amesema kati ya watu 500 wanaotumia vyoo vya kukaa, Alikuta 10 wamepatwa na Bawasiri.

Kati ya waathirika 10, Watano walikiri kuwa wamekuwa wakitumia muda mrefu kujisaidia, Huku wakichati na kuongea na simu.

FAHAMU ZAIDI KUHUSU UGONJWA WA BAWASIRI.

BAWASIRI ni ugonjwa unaojitokeza katika njia ya haja kubwa, hujitokeza kama uvimbe au kijinyama ambacho huweza kuonekana hadi nje. Kwa Kiingereza ugonjwa huu huitwa Haemorrhoids au piles.

Hakuna sababu ya moja kwa moja inayojulikana kisayansi kwamba ndiyo husababisha bawasiri, bali mambo yafuatayo yanaweza kukufanya ukapata ugonjwa huu:

  • Kufunga choo au kupata choo kigumu kwa muda mrefu
  • Ujauzito; wakati wa ujauzito watu wengine wanaweza kupatwa na bawasiri sababu ya msukumo wa mtoto karibu na sehemu ya kutolea haja kubwa.
  • Kushiriki mapenzi kinyume na maumbile
  • Uzee; kadri miaka inavyosogea ndivyo inavyokuwa rahisi kwako kupatwa na ugonjwa huu kwa baadhi ya watu.
  • Sababu za kurithi; baadhi ya watu wanaweza kurithi udhaifu wa ukuta huo wa njia haja kubwa ingawa ni kwa asilimia ndogo.
  • Kuharisha kwa muda mrefu.
  • Kutumia vyoo vya kukaa.
  • Kunyanyua vyuma vizito.
  • Mfadhaiko
  • Uzito na unene kupita kiasi

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents