Habari

Wanaokiuka marufuku ya kutembea usiku Rwanda, wapelekwa kukesha viwanja vya michezo

Katika juhudi za kukabiliana na kusambaa zaidi kwa virusi vya corona, Rwanda imeweka kanuni na sheria mbalimbali ikiwa ni pamoja na marufuku ya kutembea nje baada ya saa tatu za usiku.

Rwanda National police

Marufuku ya kutotembea usiku(curfew), si jambo geni kulisikia hususan nyakati hizi za janga la Covid-19, lakini la kushangaza ni adhabu inayotolewa kwa wale wanaokiuka marufuku hiyo.

Ukikutwa na polisi ukizurura bila sababu ama kwa miguu au unaendesha gari baada ya saa tatu za usiku moja kwa moja unaongozwa na maafisa wa polisi taratibu hadi katika moja ya viwanja vya michezo.

Huko utakesha ukielimishwa juu ya hatari na ubaya wa virusi vya corona pamoja na njia za kujiepusha na virusi hivyo mpaka asubuhi.

Mfano mapema mwezi huu watu zaidi ya 2000 walikamatwa kwa ushirikiano wa maafisa wa polisi na maafisa wengine wa serikali kwa kukiuka marufuku hiyo katika maeneo mbalimbali ya nchi na wote walilala katika viwanja mbalimbali vya michezo nchini humo huku wakipigwa na baridi na kupata darasa juu ya virusi vya corona kutoka kwa maafisa wa afya na polisi.

Maafisa wanaamini kuwa mbinu hii itawazuia watu kukiuka marufuku ya kutotoka nje wakati wa usiku na hivyo kupunguza maambukizi zaidi ya Covid-19.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents