Habari

Wanaomuunga mkono Rais Kenyatta waandamana nchini Kenya

Wafuasi wa Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta leo mchana wameandamana nje ya mahakama kuu mjini Nairobi, wakiitaka tume ya kitaifa inayoajiri na kufuatilia mienendo ya majaji iwachunguze.

Waandamanaji

Taarifa kutoka kwenye Vyombo vya Habari nchini Kenya, zimeripoti kuwa Wafuasi wa Chama cha Jubilee kinachoongozwa na Rais Uhuru Kenyatta waliandama kwa amani huku wakiwashutumu majaji wa mahakama kuu kwa kuwaibia ushindi wao kwa kufuta matokeo.

SOMA ZAIDI-Nina hasira mahakama haikunitendea haki – Rais Uhuru Kenyatta

Maandamano hayo yamefanyika baada ya gazeti la The Standard kuchapisha taarifa ya madai kwamba majaji wawili wa Mahakama kuu , Philemona Mwilu na Isaac Lenaola, ambao walipigia kura kubatilishwa kwa uchaguzi, walikutana na mawakili wa kiongozi wa upinzani, Raila Odinga, wakati wa kusikilizwa kwa kesi ya kupinga ushindi wa Bwana Uhuru Kenyatta.

Taarifa hiyo iliyotawala mazungumzo ya raia wa Kenya kwenye mtandao wa Twitter,pia inasema kuwa kuna mazungumzo ya simu yaliyo rekodiwa kuthibitisha kwamba kulikuwa na mawasiliano baina ya majaji na mawakili wa upinzani waketi kesi hiyo ikiendelea.

Majaji wa mahakama kuu mapema mwezi huu walitoa uamuzi wa kubatilishwa matokeo ya uchaguzi wa urais uliofanyika tarehe 8 Agosti yaliyompatia ushindi Bw. Kenyatta baada ya kusema kuwa mchakato wake ulitawaliwa na ukiukwaji wa haki na sheria.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents