Michezo

Wanaoongoza kwa ufungaji VPL

Ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara inatarajia kuendelea tena Alhamisi ya wiki hii kwa klabu ya Simba SC kucheza dhidi ya Mbao FC mchezo namba 25 utakao chezwa katika dimba la CCM Kirumba Mwanza.

Jumla ya michezo nane itapigwa katika viwanja mbalimbali huku mpaka sasa tayari timu hizo zimeshaingia uwanajani katika raundi tatu toka kuanza kutimua vumbi kwa ligi hiyo Agosti 27 mwaka huu.

Mpaka sasa jumla ya mabao 21 yamefungwa katika ligi kuu huku mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda na klabu ya Simba, Emmanuel Okwi ndiye anaye ongoza katika safu ya ufungaji ambapo mpaka sasa ameshafunga jumla ya mabao 6 kati ya hayo.

Wanaongoza kwa ufungaji wa mabao msimu huu wa 2017/18 wa ligi ya Vodacom Tanzania Bara.

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents