Aisee DSTV!
SwahiliFix

Wanaopiga muziki kwenye Magari, Kitchen party na Harusini kuanza kuwalipa wasanii (+video)

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe ametangaza kuwa kuanzia sasa, Watu wanaopiga nyimbo za wasanii wa muziki kwenye magari, kitchen party na harusini wataanza kuwalipa wasanii husika kwa kufuata utaratibu utakaowekwa.

Waziri Mwakyembe amesema huu sio wakati wa unyonyaji kama ilivyokuwa awali, Ambapo watu walikuwa wanakula jasho la wasanii bila aibu.

Waziri Mwakyembe ameyasema hayo jana kwenye mkutano na Wasanii wa muziki,  Waigizaji na wadau wa sanaa wa kujadili gawio la mirabaha na mapendekezo ya kuziunganisha Taasisi za BASATA, COSOTA na Bodi ya Filamu.

“Leo (Jana Agosti 28) ni mwisho kuburudika na kazi ya sanaa bila kuchangia chochote, kwenye kumbi zote iwe Harusi au kitchen party utachangia na hii si Dar es salaam bali ni nchi nzima maana huwezi kumlipa MC million 2 au 3 na usichangie hata 5% kwa muziki unaotamba nao kwenye sherehe hiyo,”amesema Waziri Mwakyembe.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW