Wanaosema nimebadilika ntawafurahisha very soon – Ben Pol

Wanaosema nimebadilika ntawafurahisha very soon - Ben Pol

Mkali wa R&B kutoka Tanzania Ben Pol amefunguka A-Z kuhusiana na maneno yanayoendelea mtaani kuwa kwa sasa msanii huyo amebadili aina ya mziki anaoufanya.

Maneno hayo yamezuka baada ya Ben Pol kufanya mziki ambao umekosa ladha ya mwanzo pia ni aina ya mziki ambao unachuja ndani ya miezi kadhaa tu tofauti na zamani ambapo alikuwa akitoa wimbo unachukua muda mrefu kuendelea kufanya vizuri katika midia.

Msanii huyo amefunguka na kusema kuwa yeye hajabadilika bali soko zima la mziki wa Bongo limebadilika,zaidi likijikita katika mziki wa biashara.

Ben Ameongeza wanaosema nimebadili aina ya mziki yani nimeacha mziki ulionitoa watafurahi muda sio mrefu,”Wanaosema hivyo ntawafurahisha very soon”ameongea hayo katika mahojiano aliyofanya na Bongo5 katika show ya “In Love & Money” iliyoandaliwa na Wasanii wawili wakubwa ambao wapo kwenye mahusiano ya kimapenzi Juma ‘Jux’ pamoja na Mwanadada Vanessa Mdee,iliyofanyika katika Ukumbi wa Nextdoor Arena Jijini Dar Es Salaam.

Lakini mbali na kuzungumzia hilo ametaja kolabo zake alizofanya na wasanii kutoka nje mfano kolabo zake na wasanii wa Nigeria kuwa zimesaidia sana kwani zimemueka sehemu nzuri ambayo anafanya vizuri katika baadhi ya nchini za kiafrika hasa kwa upande wa Afrika mashariki na Afrika magharibi.

Ben Pol amefanikiwa kufanya baadhi ya kolabo na wasanii kutoka Nigeria mfano Kizz Daniel,Chidima,na Mr Eazi

 

By Ally Juma.

Related Articles

One Comment

Bongo5

FREE
VIEW