Habari

Wanaotoka vyama vingine kuja CCM ni watu wanaojua shida za wananchi – Polepole

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole, amedai kuwa watu ambao wamekuwa wakikihama chama hiko ni wale waliotosheka lakini wale ambao wamekuwa wakihamia ni watu wa kawaida ambao wanafahamu shida za wananchi.

Akiongea na Azam Two, Katibu huyo amesema, “Watu wanaotoka CCM kwenda vyama vingine ni watu waliotosheka na wale wanaotoka vyama vingine kuja CCM ni watu wa kawaida na hawa ndio wanaokaa na kujua shida za wananchi.”

“CCM tumeweka misingi migumu itakayowabana wasiotosheka na wasio na kuasi. Tumeamua kuweka sheria ya mtu mmoja cheo kimoja,” ameongeza.

Hapo jana CCM kupitia mkutano wake mkuu wa NEC ilifanikiwa kuwapokea wanachama nguli sita kutoka vyama vya upinzania akiwemo Mwenyekiti wa BAVICHA, Patrobas Katambi, Lawrence Masha, Albert Msando, Edna Sunga, Samson Mwigamba na Profesa Kitila Mkumbo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents