Burudani ya Michezo Live

Wanaozungumzwa zaidi katika usajili barani Ulaya hawa hapa, baba wa Neymar asisitiza hili kwa mtoto wake

Manchester United inaweza kushawishika kujaribu kumrejesha tena mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic ndani ya Old Trafford.

Manchester united wanaweza kushawishika kumrejesha Zlatan Ibrahimovic kikosini

Ibrahimovic mwenye umri wa miaka 38 mchezaji wa kimataifa wa Sweden atakuwa huru kutokana na kwamba mkataba wake na klabu ya ligi ya MLS – LA Galaxy unakaribia kumalizika. (TuttoMercatoWeb, via Mail)

Meneja wa zamani wa Spain Luis Enrique, ambaye amekuwa akihusishwa na tetesi za kuwa meneja mbadala atakayechukua nafasi ya Emery katika klabu ya Arsenal, hatafikiria kurejea kwenye utawala kwa sasa . (ESPN)Emery

Aliyefikiriwa kuchukua nafasi ya Emery katika Arsenal hafikirii kurejea katika nafasi ya utawala wa klabu hiyo

Tottenham watamuhamisha winga wa Ajax na Morocco, Hakim Ziyech, mwenye umri wa miaka 26, wakati ambao Mchezaji wa kimataifa wa Denmark Christian Eriksen, mwenye umri wa miaka 27, ataondoka katika klabu hiyo. (90min)

Baba yake mchezaji wa kimataifa wa Brazil Neymar anasema kuwa hatafanya mazungumzo na Barcelona juu ya kurejea kwa mwanae katika klabu ya Nou Camp na kwamba mchezaji huyo wa safu ya mashambulizi mwenye umri wa miaka 27 atabaki katika klabu ya Ufaransa ya Paris St-Germain. (ESPN Brazil, via Mail) Baba yake Neymar anasema kijana wake ataendelea kubakia Paris St-Germain.

Image result for neymar and his father at psg

Neymar akiwa na baba yake

Kiungo wa kati wa Chelsea na Ufaransa N’Golo Kante, mwenye umri wa miaka 28, amekana taarifa zinanazomuhusisha na kuhamia katika klabu ya Real Madrid na anasema kuwa anaweza kumalizia taaluma yake ya soka katika Stamford Bridge. (Sun)

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW