Michezo

Wanariadha watwaa Medali 10 nchini Uganda

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ,Dk Harisson Mwakyembe amewapongeza wanariadha waliyoshiriki mashindano ya Shirikisho la Michezo Afrika Mashariki (FEASSA) yaliyofanyika nchini Uganda na kufanikiwa kurudi na Medali.

Wanariadha hao ambao ni vijana wa dogo wameshiriki katika michezo zaidi ya mitano huku wakikimbia katika mbio za mita 100,200 na 400.

Katika mbio zote hizo za mita 100,200 na 400 wameshika nafasi ya tatu na hivyo kuitoa Tanzania kimasomaso  miongoni mwamataifa sita yaliyoshiriki kwa kushika nafasi ya tatu.

Akizungumza na wanariadha hao Wazir Mwakyembe amewataka kujituma zaidi ilikuwa mabingwa wa dunia siku zijazo na kuiwakilisha taifa.

“Tuliwatuma muiwakilishe nchi kwenye mashindano ya shule za sekondari za Afrika Mashariki mmeitendea haki bendera yetu”,amesema Waziri Mwakyembe.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents