Fahamu

Wanasayansi nchini Uingereza na Malaysia wameugundua mti huu mrefu zaidi duniani

Wanasayansi nchini Uingereza na Malaysia wanasema kuwa wamegundua mti mrefu zaidi duniani wenye urefu wa zaidi ya mita 100. Mti huo wa kitropiki aina ya meranti ulipatikana katika msitu wa Borneo na kundi moja kutoka chuo kikuu cha Nottingham mwaka uliopita.

Kwa mujibu wa BBC. Watafiti kutoka katika chuo kikuu cha Oxford walifanya utafiti huo kwa kutumia kamera zisizokuwa na rubani kuthibitisha rekodi hio.

Mti huo uliopatikana katika eneo la uhifadhi la Danum Valley huko Sabah umepewa jina Menara ambalo linamaanisha jumba refu.

Mkweaji miti kutoka eneo hilo, jami ambaye aliupima mti huo kwa kutumia kamba alisema alliogopa kuupanda mti huo

”Lakini kwa kweli picha kutoka juu ilikuwa nzuri mno. Sijui cha kusema isipokuwa tu ulikuwa uzoefu mzuri sana”, liongezea.

Inadaiwa kuwa mti huo unaweza kuwa mti mrefu wenye maua duniani.
Image captionInadaiwa kuwa mti huo unaweza kuwa mti mrefu wenye maua duniani.

Daktari Doreen Boyd, kutoka chuo kikuu cha Nottingham, alisema kuwa ugunduzi huo ulikuwa muhimu kwa kuwa ni sayansi inayosema miti kama hii inapatikana , ni mirefu hali ya kwamba hatukuwahi kudhania na huenda kuna miti mirefu zaidi ambayo haijagunduliwa.

”Inatuambia kwamba tunahitaji kuilinda miti”, alisema. Daktari Alexander Shenkin , kutoka chuo kikuu cha Oxford , alisema baada ya kusikia ugunduzi huo walitembea kwa muda wa saa tatu hadi Menara.

Alisema: Nimeona kile ambacho wanasema ni miti mingi , lakini nilipotembea hadi katika mti huu, kichwa changu kilizidi kuangalia juu unapokaribia kileleni.Sijawahi kuona mti mrefu kama huu.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents