Habari

Wanasayansi wagundua sayari nyingine 7 zinazofanana na dunia

Wanasayansi kutoka shirika la Marekani la masuala ya anga la NASA wakishirikiana na wengine kutoka Uingereza na Ubelgiji wamegundua sayari nyingine saba ambazo zina ukubwa unaofanana na dunia.

Wataalamu hao wamegundua kuwa sayari hizo saba zinaizunguka nyota inayojulikana kama Trappist One.

Wakati huo huo imedaiwa kuwa sayari tatu kati ya hizo saba zimegundulika kuwa kuna uwezekano wa viumbe hai kuishi kwa kuwa kuna huduma muhimu yakiwemo maji.

Hata hivyo changamoto ambayo kwa sasa wanakabiliwa nao wanasayansi hao ni uwezo wa kuzifikia sayari hizo ambazo ambapo inadaiwa kuwa mpaka kuzifikia kutokana na umbali uliopo ni miaka 40 ya mwanga (speed ya mwanga).

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents