Habari

Wanaume 10 wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja (USHOGA) watiwa mikononi mwa Polisi

Wanaume wapatao 10 ambao wanatuhumiwa kujihusisha na ushoga visiwani Zanzibar wamekamatwa na Jeshi la Polisi katika fukwe za Pongwe.

Image result for Vitendo vya ushoga

Taarifa za kukamatwa kwa watu hao, zimethibitishwa na Kamanda wa polisi wa Kusini Unguja, Suleiman Hassan ambapo amesema taratibu za kisheria na kiuchunguzi zitafuatwa.

Wiki iliyopita Kampeni ya kutokomeza ushoga ilitangazwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam, Mhe. Paul Makonda, lakini hata hivyo baadae Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Mambo ya Nje ilitoa tamko kuwa kampeni hiyo hawaifahamu na ni mtazamo wa mtu mmoja yaani Makonda.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents