Habari

Wanaume 141 wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja wakamatwa Indonesia

Polisi nchini Indonesia wamewakamata wanaume 141 ambao walikuwa wanahudhuria sherehe ya wapenzi wa jinsia moja katika mji mkuu wa Jakarta, siku ya Jumapili.

Mapenzi kati ya watu wa jinsia moja sio marufuku kulingana na sheria za Indonesia, isipokuwa katika mkoa wa kihafidhina wa Aceh.

Msemaji wa polisi wa Jakarta Raden Argo Yuwono alisema kuwa baadhi ya wale waliokamatwa wanaweza kushitakiwa chini ya sheria kali ya Indonesia ya kupambana na vitendo vichafu.

Polisi wanasema kila aliyehudhuria, akiwemo raia mmoja wa Uingereza na mwingine wa Singapore walilipa kiingilio cha rupi elfu 185 (Dola 14; Pauni 10).Wiki iliyopita, wanaume wawili walihukumiwa kuchapwa viboko mbele ya umma katika mkoa wa Aceh, baada ya kupatikana wakifanya ngono.

Sheria kali dhidi ya uhusiano wa kimapenzi kati ya watu wa jinsia moja zilianza kutekelezwa nchini humo mwaka wa 2014.

Na Laila Sued

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents