BurudaniHabari

Wanaume Halisi hawa hapa

Juma Nature“Mshike mshike ndege tunduni, Si wajanja tumekimbia, Mshike mshike ndege tunduni, Waliobaki wataumia…

Juma Nature“Mshike mshike ndege tunduni,

 

Si wajanja tumekimbia,

 

Mshike mshike ndege tunduni,

 

Waliobaki wataumia,

 

Mshike mshike ndege tunduni,

 

Hatuogopi wakivamia…. hiki ni kiitikio cha wimbo mpya wa TMK halisi kundi linaloongozwa na msanii Juma Nature ujulikanao kwa jina la ‘Ndege tunduni’ nah ii ni baada ya kujiengua na waliokuwa washkaji zake, kweli machizi wamekamua kinoma na madhui ni full kuwalenga hawa wanaojiita wanaume nao .

 

“Wanaume ni yangu, kundi ni langu, nembo ni yangu, na mimi ndio mzawa halisi TMK hivyo siwezi kufelishwa na watu ambao naamini hawaniwezi” alisema Sir Nature kwa njia ya simu alipokuwa mkoni Dodoma kwenye ziara maalum kwa ajili ya kuinadi timu yake mpya ya wanaume halisi”

 

Kundi hilo jipya ambalo linawakutanisha wasanii kama D-chief, Rich One, Bk, Dollo, Inspekta Haroun na Qiblah mwenyewe, ambapo mpaka sasa wameshapiga show nane na baada ya hapo wanatarajia kuelekea nchini Mozambique kisha Afrika Kusini kwa ajili ya kupiga show mbili tatu.

 

Source: Bongo5

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents