Habari

Wanaume wanaotelekeza watoto kukiona cha mtema kuni!

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda Alhamisi hii ametangaza kiama kwa wanaume wenye michezo ya kuwazalisha wanawake kisha kuingia mitini kwa kukwepa majukumu ya kulea mtoto jambo linalosababisha ongezeko la watoto wa mitaani na ombaomba.

RC Makonda amesema anataka kuongezea nguvu Idara ya Ustawi wa Jamii kwa kuuunda kamati ya wanasheria wabobezi kwaajili ya kuwapeleka mahakamani wanaume wanaotelekeza familia na kuwaachia wanawake mzigo wa malezi.

Aidha amesema kuwa Kamati hiyo pia itafanya marekebisho ya sheria ya pesa ya matunzo ya mwezi kwa mtoto kisha kuwasilishwa bungeni kwakuwa pesa inayotolewa ni ndogo na haiendani na maisha ya sasa.

Amesema ni lazima ifike mahala mwanaume anaposababisha ujauzito kwa binti atambue analojukumu la kuhudumia.

Amesema hayo wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi za Vifaa vya Ultrasound 10 za kisasa Aina ya “GE Vscan Access” zenye thamani ya zaidi ya shilingi Million 150 kwa Hospital 10 zilizofanya vizuri katika kutoa huduma bora za Afya na kupunguza vifo vya Mama na Mtoto wakati wa kujifungua.

Amezipongeza Hospital, Zahanati na Vituo vya Afya vilivyofanikisha Mkoa wa Dar es Salaam kuwa kinara wa huduma bora za Afya na Kupunguza Vifo vya Mama na Mtoto na kuwaasa Watoa huduma kuwa na lugha nzuri kwa Wagonjwa.

Kwa Upande wake Mshauri Mtaalamu wa Magonjwa ya Mama na Mtoto kutoka CRDB Dr BRENDA DIMELLO amesema Dar es Salaam imekuwa Mkoa wa kwanza kupunguza vifo vya Mama na Mtoto kutokana na usimamizi thabiti wa RC MAKONDA na watendaji wa Afya.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents