Burudani

Wanaume Waoneshana ubavu

Kila mshabiki wa muziki wa bongo fleva aliweza kuwa na lake la kusema kuhusiana na mpambano ambao ulikuwa ukisubiriwa kwa hamu kubwa baina ya mahasimu wawili yaani TMK Wanaume na Wanaume Halisi ambao ulifanyika Ijumaa ilyopita…

Juma Nature


 


Kila mshabiki wa muziki wa bongo fleva aliweza kuwa na lake la kusema kuhusiana na mpambano ambao ulikuwa ukisubiriwa kwa hamu kubwa baina ya mahasimu wawili yaani TMK Wanaume na Wanaume Halisi ambao ulifanyika ndani ya ukumbi wa Dimond Jubilee Ijumaa ilyopita ambapo ni dhahiri ukumbi huo ulionekana kuwa mdogo kutokana na umati mkubwa ambao ulihudhuria ukumbini humo.



Mahasimu hao waliweza kulishambulia jukwaa kikamilifu na kila mmoja alionekana kujiandaa kikamilifu ambapo upande wa TMK Wanaume uliongozwa na Mheshimiwa Temba wakati safu ya Wanaume Halisi iliongozwa na Sir ‘Juma’ Nature, Eh bana shughuli ilikuwa si ya kitoto kwani mashabiki ndio walisimama kidete kudhihirisha nani ni mshindi katika onesho hilo.


 


Foleni
Foleni ndefu ya kuingilia ukumbini 


 



Wanaume Halisi ndio waliofungua mpambano huo kwa kupandaa jukwaani na mikono fulani ambayo ni maarufu na kuufanya umati kudata mapema kabla hata mambo hayajachanganya ambapo masongi kama ‘Nje ndani ya gangwe Mobb na Hili Game ya Juma Nature yalionekana kufanya vizuri ile mbaya na kuupagawisha umati uliohudhuria.



Upande wa TMK Wanaume hali ilionekana kujikongoja kwani wlitimba Jukwaani na singo yao ‘Pisha Njia’ na mashabiki walionekana wakirusha makopo ukumbini huku wakionesha ishara ya tatu bila, jambo ambalo lilionekana kuwa watoto wa Saidi Fellah walizidiwa kidogo.



Kwa ujumla Show ilikuwa na kila mmoja upande ulifanya vizuri hasa kwenye ngwe ya mwisho ambayo Yowe la kufa mtu lilisikika wakati Nature na vijana wake walipokamua ‘tatu bila’ jukwaani hakuna aliyekaa na kuvumilia kushangilia, halikadhalika vijana wa Fellah walisimama kidete kujitetea na madaluga yaliyokuwa yakiwafikia walipotwanga msumari wao ‘dar mpaka moro’.




Onesho hilo lilidhaminiwa na kampuni ya sigara, bia ya Kilimanjaro, Prime Time Promotion na pamoja na Tigo ambao ndio walikuwa wakuu wa onesho hilo, hadi mwisho wa shughuli kila aliyetimba ndani ya Diamond aliweza kujaji mwenyewe na kujua nani alikuwa mkali baina ya mahasimu hao.


 


Bofya hapa kupata videoclips za mpambano


 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents