Michezo

Wanawake 28 ‘wapikwa’ na TFF, KTO

Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) kwa kushirikiana na Taasisi ya Karibu Tanzania (KTO), hii leo wamehitimisha kozi ya ukocha kwa wanawake.

Kozi hiyo iliyochukua siku mbili imejumuisha wanawake 28, kutoka katika vyuo mbalimbali vya Maendeleo ya Jamii.

Kozi hiyo iliyofanyika katika uwanja wa Karume zinakuwa kozi za pilikufanyika kwa makocha hao.

Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo, Yusuph Singo amesema Serikali inafahamu kuwa inatakiwa kuwekeza kwenye soka la wanawake kuanzia upande wa vijana na ndio maana inatengeneza mazingira na sera zitakazowezesha mafanikio hayo.

Singo amesema nchi mbalimbali wana maendeleo makubwa katika mpira wa miguu kwa wanawake na sasa wakati wa Tanzania kuwekeza katika upande huo kuanzia kwa watoto na makocha.

Kwa upande wa mwenyekiti wa chama mpira wa wanawake ‘TWFA,’ Amina Karuma amesema lengo la chama chake na TFF ni kuhakikisha soka linachezwa nchi nzima na kuwataka wahitimu hao kuvitumia vyeti walivyovipata kuendeleza soka la wanawake na kufanyia kazi yale yote waliyofundishwa.

Wakati Mkurugenzi wa ufundi wa ‘TFF’, Salum Madadi amesema kufundisha watoto kuna changamoto nyingi, lakini makocha hao wamefundishwa maarifa ya jinsi ya kukabiliana nazo.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents