Habari

Wanawake wa Dar waliotelekezwa na wanaume zao kusaidiwa na RC Makonda

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda amewatangazia wawanake wote waliotelekezwa na waume zao na hawapatiwi fedha za matunzo ya mtoto kufika ofisini kwake siku ya Jumatatu ya April 09 kwaajili ya kupatiwa msaada wa kisheria.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na ofisi ya RC, inasema Jopo la wataalamu wa Sheria, Maafisa Ustawi wa jamii na Askari Polisi kutoka Dawati la Jinsia wamejipanga ipasavyo kukuhudumia na kuhakikisha mzazi mwenzio anatoa fedha za matunzo ya Mtoto.

“Ewe mwanamke huu sio wakati wa kulia wala kuteseka, serikali yako itasimama na wewe kuhakikisha unapata haki yako uliyoikosa kwa muda mrefu,” Taarifa hiyo inaeleza.

Alisema Huduma hii inatolewa bure chini ya uongozi thabiti wa serikali ya awamu ya tano.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents