Habari

Saudi Arabia kuruhusu wanawake kuendesha magari

Serikali ya Saudia Arabia imetoa ruhusa kwa wanawake nchini humo kuendesha magari.

Idhini hiyo imetolewa na Mfalme Salman bin Abdulaziz, na itabaki kuwa historia kwa taifa hilo. Uamuzi huu umefikiwa kutokana na harakati za muda mrefu kwa makundi ya wanawake na haki za bindamu kushinikiza wanawake waruhusiwe kuendesha magari.

Saudi Arabia imekuwa nchi pekee Duniani kuwazuia wanawake kuendesha magari kwa muda mrefu, Abdallah al-Mouallimi Mwakilishi wa umoja wa mataifa kutoka Saudia ametangaza habari hizi.

Sheria hii inaanza kufanya kazi mwezi June mwakani, na kwa sasa Wizara itatakiwa kuandaa ripoti maalumu kuhusiana na jambo hilo.

 

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents